Rorya

Mkomboe CBO support

MRADI WA UFUGAJI KUKU, NYUKI, SAMAKI NA KILIMO CHA MBOGA MBOGA

(Vijiji husika: Kyamwame, Nyamonga na Etaro) – Wilaya Rorya na Msoma vijijini)

Mradi huu wa ufugaji kuku, nyuki, samaki na kilimo cha mboga mboga unatekelezwa na shirika la Mkomboe katika vijiji vitatu vya kyamwame, Nyamunga (vilayani Rorya) na Etaro (wilayani Musoma vijijni) chini ya ufadhiri wa Tanzania Association of Environmental Engineers (TAEEs) ambao ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na maswala ya uhifadhi Mazingira nchini.

Ufadhiri wa kwanza kwa shirika la Mkomboe ulianza mwaka 2010-2011 kwa kusaidia mradi mmoja tu wa ufugaji kuku wa mayai ambapo kikundi kilifanikiwa kufuga kuku 300. Awamu ya pili ilikuwa 2013-14 ambapo ilipanua maeneo ya ufadhiri kuongezea miradi ya ufugaji samaki, kilimo cha bustani (mboga mboga) na ufugaji wa nyuki. Awamu ya kwanza ilifadhiri kiasi cha Sh. 4,400,000/= wakati awamu ya pili uliongezeka baada ya kuongeza idadi ya miradi toka mmoja wa awali na kufikia mine na katika maeneo matatu zaidi na hivyo kupelekea ufadhiri huu kufikia Tshs16,970,050/= ambapo zimekuwa zikitolewa kwa awamu kama sehemu ya kusimamia utekelezaji bora wa miradi hii. Kwa undani wa utekelezaji wa mradi huu soma ripoti hapa