Ziara ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwenye miradi ya maji wilayani Karagwe na Kyerwa

Mkuu wa Mkoa wa Kagera ndugu John Mongela aliamua kutembelea wilaya ya Kyerwa na Karagwe mnamo tarehe 29/1/2015 na 31/1/2015.Ziara ya mkuu wa Mkoa ililenga kutembelea miradi ya maji na ujenzi wa maabara wilayani Karagwe na Kyerwa.

Jambo la kufurahisha katika ziara hii ni kwa jinsi maandalizi ya mapokezi ya Mkuu wa Mkoa huyu yalivyowafanya watendaji wengi wa Serikali kujipanga na kuhakikisha zira ya mkuu wa mkoa haitaibua jambo lolote ambalo lingeweza kuwa surprise kwao,Watendaji wengi wa Sekali wilayani Karagwe na Kyerwa hawana tabia ya kuitembelea miradi na kujiua kwa kina na mara nyingi huwa wanapewa taarifa tu jinsi miradi inavyotekelezwa.Lakini wakati Mkuu wa Mkoa alipoahidi kutembelea Wilaya hizi mbili, basi wiki moja kabla ya ujio wake watendaji wakuu wote na kamati mbalimbali walikua wanatembelea mradi  mmoja kwenda mwingine na kuijua kwa kina.

Ofisi yetu ya TAEEs Karagwe pamoja na timu nzima ya TAEEs Karagwe  ilitoa ushirikaiano wa hali ya juu katika kuhakikisha watendaji hawa wa Halmashauri pamoja na kamati mbalimbali wanapata yale waliyokua wanayahitaji kutoka kwetu.

Mradi wa Kigorogoro

Mnamo tarehe 29/1/2015 Mkuu wa Mkoa alianzia kutembelea mradi wa Kigorogoro na alifika katika mradi saa nne asubuhi.Kwa upande wa TAEEs Mhandisi mkaazi alifika kwenye mradi saa tatu na nusu asubuhi kwa ajili ya kutoa maelezo au kujibu hoja zitakazotokana na mradi kwa Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa mkoa alifika eneo Tenki la maji la ujazo wa 135m3 na alipata taarifa ya mradi wa Maji kutoka kwenye ofisi ya Maji Kyerwa na baada ya hapo Mkuu wa Mkoa alisifia kazi inavyokwenda na kumpongeza Mkandarasi na Msimamizi wa ujenzi kwa kazi nzuri ya ujenzi wa tenki lenye Ubora wa hali ya juu.Jambo ambalo alilizungumza ambalo lilionyesha kweli kazi ni bora ni pale aliposema Atalichukulia tank hilo kama mfano katika mkoa wa Kagera kwani lina ubora wa hali ya juu,na kokote atakakokwenda atalitolea mfano tank la Kigorogoro kama tank bora. Baada ya maelezo hayo aliuliza uwepo wa kamati ya maji na kama wanaendelea kuchangisha michango ya maji.Kamati ilionekana ipo na wanendela kuchangisha michango.

Mradi wa Maji Rwabikagati.

Baada ya mradi wa Kigorogoro Mkuu wa Mkoa alielekea kukagua mradi wa maji Rwabikagati.Lakini pia alikua akikagua ujenzi wa maabara kwenye Kata zilizoko katikati ya Kigorogoro na kijiji cha Rwabikagati.Alifika kwenye mradi wa Rwabikagati kwenye majira ya saa tisa na nusu alasiri,alifikia eneo la tenk la maji lilipojengwa.Alipata taarifa ya mradi toka ofisi ya maji Kyerwa na baadae akahoji maswali yafuatayo

  1. Aliwahoji wananchi kama wanapata huduma ya maji
  2.  Kwanini mradi haujakabidhiwa mpaka saa hivi wakati watu wanaendela kupata huduma.
  3.  Matengenezo madogo madogo yanafanywa na nani?
  4.  Kwanini makandarasi hayupo site.

Majibu.

Swali la kwanza alilijibu mwenyekiti wa kamati ya maji na kusema huduma inapatikana vizuri na watu wanapata huduma ya maji takribani miezi mitano sasa.

Swali la pili lilijibiwa na Mhandisi Mkaazi toka TAEEs ambapo alitoa maelezo kuwa mradi haujakabidhiwa kwasababu kuna vitu vidogo vidogo havijakamilishwa na Mkandarasi ambapo anahitaji kuvikamilisha halafu mradi uingie chini ya uangalizi wa miezi 6 ndipo ukabidhiwe.

Swali la tatu lilijibiwa na Mhandisi Mkaazi toka TAEEs ambapo alitoa maelezo kwamba Mradi una fanyiwa matengenezo madogo madogo na Fundi wa mradi ambaye alipewa mafunzo na Mkandarasi toka mradi unaanza mpaka ulipokumilika.Fundi huyu hufanya matengenezo lakini kwa gharama za Mkandarasi kwa kuwa bado mradi uko chini ya Mkandarasi.

Swali la nne lilijibiwa na Mhandisi Mkaazi toka TAEEs kuwa Mkandarasi amaendoka kwani amekamilisha mradi asilimia 98 na anaidai Halmashauri takribani milioni 200 ambazo halmashauri imeshindwa kumlipa mpaka sasa.Alishindwa kuendelea kuwa site kwani gharama zingeongezeka zaidi kama angeendelea kuwepo wakati hajalipwa malipo yake.

Baada ya majibu hayo ya Maswali ya Mkuu wa Mkoa, Diwani wa kata ya Murongo ambayo kijiji cha Rwabikati ni moja ya vijiji vyake alitoa hoja kuwa Pamoja na watu kupata huduma ya maji lakini mradi una tatizo kwani Mashine ya kuungia mabomba (Fusion machine) ni nzito na kunapokua na tatizo linalohitaji mashine itumike basi mafundi wanapata shida sana kuibeba.

Mkuu wa Mkoa alihoji hiyo mashine ikoje upande Msimamizi  wa mradi na akapewa majibu ambapo baada ya majibu hayo,Mkuu wa Mkoa alimwambia Diwani  kuwa mambo yamebadilika na Mashine hiyo ni teknologia mpya na wananchi wachangie gharama za kuisogeza mashine hiyo pale inapohitajika.

Pia Mkuu wa Mkoa akahoji Wananchi na Diwani kama toka wameanza kutumia huduma ya maji wanachangia kwa ajili ya uendeshaji wa mradi.Majibu ya swali hili ilikua ni Hapana na Diwani akasema hawachangii kwasababu bado hawajakabidhiwa mradi.

Mkuu wa Mkoa alitoa agizo la mara moja kuwa huo ni uzembe na michango ianze mara moja kuanzia siku hiyo.Aliendelea kusema iwapo Mkandarasi akiondoka na kuwakabidhi basi wawe wana hela yao ya uendeshaji wa mradi maana bila hivyo mradi huo utakufa.

Baada ya Hapo Mkuu wa Mkoa aliendelea na ziara za ukaguzi wa Maabara.Ziara ambayo ilikua haiihusu TAEEs

Comments are closed.

Search
Downloads
Votes

How Is Our Site?

View Results

Loading ... Loading ...